Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Euro 2024 tukutane Ujerumani

Skysports San Marino Euro Euro 2024 tukutane Ujerumani

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi 21 tayari zimefuzu ushiriki wa fainali za Mataifa ya Ulaya (Euro) 2024 zitakazofanyika Ujerumani kuanzia Juni 14 hadi Julai 14 mwakani. Mechi za mwisho zilichezwa jana na kilichobaki ni kusubiri timu zitakazoungana nazo baada ya michezo ya play off na ratiba ya makundi itakayopangwa Desemba 2, mwaka huu.

Hatua ya mchujo itahusisha timu 12 na kati ya hizo ni tatu tu ndizo zitaungana na mataifa mengine 21 kukamilisha timu 24 zitakazopambana kuwania ubingwa kwenye fainali hizo.

Katika mechi za mwisho juzi Jumanne, Ufaransa ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Ugiriki iliyomaliza nafasi ya tatu kwa tofauti ya pointi tisa na mabingwa hao wa Kombe la Dunia mwaka 2018, huku Andorra ikipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Israel.



Romania ilishinda bao 1-0 dhidi ya Uswisi iliyo nafasi ya pili kundi J, wakati Gibraltar ikichezea kichapo kingine kizito cha mabao 6-0 kutoka kwa Uholanzi.

Hicho ni kipigo cha pili kizito kwa Gibraltar kwani wikiendi iliyopita Ufaransa iliibamiza mabao 14-0.

Kosovo ilipigwa bao 1-0 na Belarus, huku Croatia ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Armenia.

Wakati huo huo, Wales imetibua nafasi ya kufuzu Euro baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Uturuki na sasa itacheza play-offs kusaka nafasi ya kushiriki Euro ili kuwafuata ndugu zao England ambao wamefuzu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live