Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Euro 2024: Uefa kuongeza wachezaji kikosi kwa mashindano Ujerumani

Euro 2024: Uefa Kuongeza Wachezaji Katika Kikosi Kwa Mashindano Ujerumani Euro 2024: Uefa kuongeza wachezaji kikosi kwa mashindano Ujerumani

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: Bbc

UEFA inafikiria kuongeza idadi ya kikosi kwa watakaoshiriki michuano ya Ulaya msimu huu nchini Ujerumani hadi kufikia wachezaji 26 kufuatia mazungumzo na makocha.

Majadiliano na wakubwa wa kimataifa ambao timu zao zilikuwa zimefuzu kwa Euro 2024 yalifanyika Dusseldorf Jumatatu.

"Uefa imezingatia maoni na mitazamo mbalimbali inayoshirikishwa," ilisema taarifa ya shirikisho la soka barani Ulaya.

"Uamuzi wa mwisho utafanywa katika wiki zijazo."

Suala hili lilijadiliwa kama sehemu ya warsha kubwa ya siku mbili kwa waliofika fainali, na sasa inakwenda kwa kamati ya mashindano ya timu ya taifa ya Uefa kisha kamati yake ya utendaji.

Vikosi kwa sasa vina wachezaji 23 pekee, kanuni zilizotumika kabla ya Euro 2020. Kwa mchuano huo, wachezaji wengine watatu walipunguzwa kutokana na athari za Covid-19 kwenye kikosi.

Taarifa ya Uefa iliongeza: "Majadiliano hayo chanya yalionyesha mitazamo tofauti kati ya makocha, wengine wakionyesha nia ya kuongeza idadi ya kikosi. Wengine walisema upendeleo wao wa kufunga kikosi cha wachezaji 23, ugumu wa kufanya mazoezi na wachezaji wa ziada, usimamizi na kuongezeka kwa gharama iliyowekwa kwa vyama vya kitaifa."

Mkufunzi wa England Gareth Southgate hapo awali alikuwa akipendelea vikosi vya wachezaji 23 lakini hivi majuzi alizungumzia upendeleo wa wachezaji watatu wa ziada.

Fainali za Kombe la FA, Ligi ya Europa na Ligi ya Mabingwa zitachezwa baada ya Southgate kutaja kikosi chake cha muda cha wachezaji 26 mnamo Mei 21.

Chanzo: Bbc