Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Etoo aburuzwa FIFA

Etoo Samuel Etoo, Rais wa Shirikisho la Soka Cameroon

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Chama cha soka cha Cameroon (FECAFOOT), Samuel Eto’o ametuhumiwa kuhusika na upangaji wa matokeo na kutoa vitisho, katika faili la kustusha lililowasilishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Fifa. Kwa mujibu wa gazeti la The Athletic, Eto’o anakabiliwa na orodha ndefu ya tuhuma zilizoelekezwa kwake zikiwamo kuhusika katika upangaji wa matokeo, kusambaza taarifa za uongo, kutoa vitisho, kusababisha vurugu na matumizi mabaya ya madaraka.

Makamu wa rais wa zamani wa Fecafoot, Henry Njalla Quan Junior amelituma faili hilo kwa Fifa na pia linachunguzwa na Caf. Shirikisho hilo la soka la Afrika pia limethibitisha kuwa linachunguza kuhusiana na madai hayo dhidi ya Eto’o na Fifa iliwahi kushauriwa kumtoa staa huyo wa zamani wa Barcelona katika nafasi yake kutokana na mfululizo wa matukio tata.

Njalla Quan Junior amedai kwamba mechi kati ya akademi yake na Kumba City FC ilipangwa matokeo na Eto’o, akieleza tukio hilo kama moja ya “kashfa kubwa kabisa maishani”. Bosi huyo wa Cameroon pia anatuhumiwa kupanga matokeo ya timu ya “rafiki yake wa karibu“ Valentine Nkwain ipande daraja. Victoria United ikapanda daraja baada ya kushinda mechi 11 kati ya 17 za mwisho wa msimu licha ya kupoteza mechi nne kati ya saba za kwanza za msimu huo.

Gazeti la The Athletic likaongeza kuwa uhusiano wa Njalla Quan Junior na Eto’o uliharibika kabisa, na ukasababisha straika huyo wa zamani kudaiwa kumlipa mtu atume meseji ya vitisho. Ilisomeka: “Mimi ni mafia wa mapinduzi haya na katika umafia huu hatuwasaliti viongozi wetu. Nimekuwa nikilinda maslahi ya mipango yetu hadi leo. Hivyo, kama utanizingua kaa tayari kubeba mzigo wa kitakachotokea.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live