Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eto’o atangaza kumng'oa Kocha wa Cameroon, Rigobert Song

Cameroun Song Et Etoo 1 Samuel Eto’o na Rigobert Song.

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la soka la Cameroon (Fecafoot), Samuel Eto’o ametangaza kuwa Rigobert Song, mkataba wake umetamatika rasmi.

Uvumi wa kufukuzwa kwa kocha huyo ulivuma tangu kuondolewa mapema kwa Cameroon, bingwa mara tano wa Afrika, mikononi mwa Nigeria katika hatua ya 16 bora ya AFCON 2023.

Rigobert Song ataondoka kwenye benchi la timu ya taifa, Rais wa Fécafoot, Samuel Eto’o ametangaza rasmi Jumatano Februari 28 katika mahojiano ya kipekee na FRANCE 24.

Hapo awali ilielezwa kuwa, Rais wa nchi ya Cameroon, Paul Biya ameamua kuingilia kati uteuzi wa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Cameroon ambao hautamhusisha Rais wa sasa wa Shirikisho la Soka nchini Cameroon (FECAFOOT) Samuel Eto'o baada ya kufeli kwenye uteuzi wa kocha wa sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live