Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eto'o aomba radhi kwa tukio la kushambulia

Samuel Etoo Apologize.png Samuel Etoo

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT), Samuel Eto'o ameomba radhi kwa tukio alilofanya la kumshambulia mtu nje ya Uwanja wa 974 Doha baada ya mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya Brazil na South Korea siku ya Jumatatu.

Etoo alionekana akimshambulia mtu huyo aliekuwa ameshikilia Camera huku akimuuliza maswali na kumrekodi.

Taarifa zinadai kuwa mtu huyo alimuuliza Etoo kuwa walimpa hongo mwamuzi kutoka Gambia ili washinde mchezo wao dhidi ya Algeria mwezi Machi ambapo Cameroon walishinda mabao 2-1 na kufuzu kwa michuano hiyo ya Kombe la Dunia.

Swali hilo lililoamsha hasira za Etoo ambae alidai mtu huyo ni mshabiki wa Algeria ambae alimdhihaki kwa kuwa walikuwa washindani wao wakati wa kuwania kufuzu kucheza Fainali hizo mwezi Machi.

Mchezo huo ulimalizika kwa Cameroon kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 hivyo Cameroon wakafuzu kwa faida ya bao la ugenini.

Cameroon imeishia hatua ya Mkaundi katika Fainali hizo zinazoendelea nchini Qatar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live