Wiki hii, Rais wa Shirikisho la soka Cameroon, Samuel Eto’o alitoa kauli ambayo ni kama alikuwa anampigia cha-puo Rais wa Shirkisho la Soka duniani (FIFA), Gianni Infantino.
Eto’o alisema Afrika itapata wakati mgumu sana iwapo Infantino akiondoka FIFA na ile thamani ambayo inapa-ta hivi sasa haitokuwepo.
Kwa maana nyingine Eto’o anashauri vyama na mashirikisho ya soka Afrika yapige kura ya ndio kwa Infantino wakati wa uchaguzi wa FIFA ili bara letu liendelee kunufaika naye pindi akiwa madarakani.
Kwa sisi tuliosoma Cuba, hiki alichokifanya Eto’o ni kuingia kwenye mfumo wa Infantino na FIFA yake na sasa ameanza kuzielewa siasa za soka tofauti na alipoingia madarakani.
Eto’o sasa amepata ufahamu hawezi kudumu kwa muda mrefu katika nafasi ya Urais wa Shirikisho la Came-roon aliyopo kwa sasa kama hatokuwa sehemu ya familia ya Infantino na hii ndio imekuwa silaha kubwa kwa viongozi wa vyama vingi vya soka.
Alikuwa na jina kubwa wakati alipokuwa anacheza soka lakini haliwezi kumbeba na kumfanya atambe kwenye uongozi wa soka kama hana ukaribu au ushikaji na waandamizi waliopo katika eneo hilo mfano ni huyo Infantino.
Hakuna namna ambayo unaweza kudumu katika uongozi wa soka kama mabosi wa FIFA au CAF hauko karibu nao na unaweza kujikuta unaondoka kirahisi kwenye nafasi yako kwa vile wao ni kama wameshikilia mpini.
Mwanzoni Eto’o alionekana kama ni jeshi la mtu mmoja kwa kutojiweka karibu na vigogo wa mamlaka zilizo juu yake kwa maana ya FIFA na CAF pengine akiamini jina lake linatosha kumfanya awe na ulinzi wa nafasi yake pale Cameroon.
Hata hivyo, baada ya kuhudumu kwa muda katika nafasi yake, sasa amefahamu mfumo ulivyo na ameshauingia.