Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eti tatizo la Brazil ni paka

Paka Brazil Eti tatizo la Brazil ni paka

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wiki iliyopita timu ya taifa ya Brazil iliendelea kupitia nyakati ngumu baada ya kutolewa katika michuano ya Copa America kwa kuchapwa na Uruguay kwa penalti 4-2.

Baadhi ya mashabiki na wataalam wa mambo wanadai huenda taifa hilo linafanya vibaya katika soka kutokana na laana ya paka.

Ndio, laana hiyo ya paka inadaiwa kutokea mwaka 2022 katika fainali za Kombe la Dunia, Qatar.

Ilikuwa ni muda ambao mchezaji wa Brazil, Vinicius Jr akifanya mkutano na waandishi wa habari, ghafla akatokea paka aliyepanda juu ya meza.

Vinicius aliona ni kama jambo la kuchekesha na wala hakuangaika naye lakini afisa wa habari wa Brazil akanyanyuka na kumnyakuwa paka huyo kisha akamtupa.

Namna alivyomtupa ilionekana kuchefua mashabiki wangi waliomkosoa ingawa paka huyo hakupata madhara yoyote.

Tangu tukio hilo litokee Brazil imekuwa ikifanya vibaya sana katika michuano mbalimbali iliyoshiriki, vilevile baadhi ya mastaa wao wakubwa wamekuwa wakipata majeraha wanapokuwa wanakaribia kujiunga na timu.

Ni hivi, Siku chache baada ya paka huyo kutupwa, Brazil iliondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia na Croatia kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.

Jambo la kushangaza ni hapo pia waliondolewa kwa penalti 4-3 kama ilivyokuwa wiki iliyopita na Uruguay.

Oktoba mwaka jana, Neymar alipata majeraha ya goti akiwa anaitumikia timu hiyo katika mchezo dhidi ya Uruguay. Jeraha hilo lilikuwa kubwa zaidi katika maisha yake ya soka, maumivu hayo yamesababisha asiwepo pia katika timu ya taifa kwenye michuano ya Copa America.

Ukiondoa hali mbaya kwa timu ya wakubwa mambo pia hayaeleweki katika kikosi chao cha vijana cha U-20 na mwaka jana kilionekana kuanza vizuri katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuichapa Tunisia mabao 4-1 hatua ya 16 bora.

Ilikuwa ikitazamiwa kufanya vizuri zaidi lakini katika hali isiyotarajiwa ikiwa inaongoza kwa mabao2 2-1 dhidi ya Israel, meza ilipinduliwa na kupoteza kwa mabao 3-2, ikatolewa hatua ya robo fainali.

Taifa hili lililobarikiwa vipaji pia lilishindwa kufuzu michuano ya Olimpiki ya Paris.

Chanzo: Mwanaspoti