Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eti Lampard anachukua hii Champions League

Frank Lampard Uefa.jpeg Frank Lampard

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Guss Hiddink anaamini Frank Lampard anaweza kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Chelsea msimu huu.

Usicheke. Lampard, 44, amebamba ajira kama kocha wa muda Chelsea na wiki iliyopita alipoteza mechi yake ya kwanza alipochapwa 1-0 na Wolves katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Hiddink, 76, naye aliwahi kuwa kocha wa muda mara mbili tofauti kwenye kikosi hicho cha Chelsea, ya kwanza ilikuwa 2009 baada ya Luiz Felipe Scolari kufutwa kazi. Aliongoza Chelsea kumaliza nafasi ya tatu kwenye ligi na kubeba taji la Kombe la FA, jambo lililowashawishi mashabiki kumtaka abaki Stamford Bridge.

Lakini, msimu ulipokwisha alirejea kwenye ajira yake ya kuinoa timu ya taifa ya Russia. Awamu yake ya pili, Stamford Bridge ilikuwa mwaka 2015 alipotua kuchukua mikoba ya Jose Mourinho. Hiddink aliongoza Chelsea kumaliza nafasi ya 10 hapo baada ya kupanda kwa nafasi sita. Aliongoza timu hiyo kucheza mechi 12 bila ya kupoteza, iliyokuwa rekodi klabuni hapo.

Na sasa Mdachi huyo anaamini Lampard atafikia mafanikio kama yake na anaamini atabamba mkataba wa kudumu Chelsea.

“Ana nafasi ya kufanya kitu kizuri hadi kufikia mwisho wa msimu kwenye hii Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nadhani anaweza kuwa mtu sahihi wa kuiongoza Chelsea mpya," alisema Hiddink.

“Nina kumbukumbu nzuri ya Frankie. Alikuwa kiongozi shupavu vyumbani. Kama mchezaji, kama kiungo mahiri. Alikuwa na nguvu, maalumu na hatari sana alipokaribia boksi. Nilikuwa sina shaka, nilijua atakwenda kuwa kocha.”

Lampard na Chelsea yake atakuwa na mtihani mzito usiku wa leo Jumatano, wakati atakapokabiliana na Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaopigwa Santiago Bernabeu.

Chanzo: Mwanaspoti