Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Estadio Benito Villamarín: Huu sio uwanja tu, ni sehemu flani ya bata

Estadio Benito Villamarin Estadio Benito Villamarín.

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna timu zinajenda Uwanja wa Mpira halafu kuna huu Uwanja wa Bennito Villamarin hakika huu sio uwanja pekee bali ni sehemu ya bata pia.   Ndio huu ni uwanja wa mpira wa miguu wa klabu ya Real Betis kutoka nchini Hispania,kwa wale wanaofuatilia soka Real Betis ni moja kati ya timu kongwe na kubwa pale nchini Spain.   Hiyo ni picha ya Uwanja huo utakavyokuwa pindi utakapomalizika kujengwa,kwa mujibu wa mpango kazi wao Uwanja huo utakamilika mwaka 2026.utaanza kujengwa upya mwaka 2024.   Unaambiwa zaidi ya wakandarasi 100 walituma picha na michoro juu ya ubunifu wa uwanja huo lakini ni mwamba Rafael De La-Hoz ndiye aliyeshinda tenda hiyo.   Unaambiwa yeye ndiye alikuwa wa mwisho kutuma mchoro wa Uwanja huo na maafisa wa Real Betis wakaupitisha moja kwa mpya.   Historia ya Rafael De La-Hoz inaonyesha kuwa ni mzaliwa wa mji wa Cordoba huko Spain na alizaliwa 1955,katika familia ya baba ambaye alikuwa ni mkandarasi mkubwa.Rafael alianza kuwa mkandarasi akiwa na miaka 17 tu.   Degree yake ya Ukandarasi alipata nchini Hispania akiwa na umri wa miaka 16 tu katika chuo cha Higher Technical School of Architecture of Madrid.   Hivyo ni kama alichukuwa mikoba ya mzee wake,Uwanja huo ukikamilika utakuwa unachukuwa watazamaji 60,000.   Zaidi ya Bilioni 190 zitatumika kuuboresha uwanja huo ambao utakuwa na kumbi 3 za starehe kwa ndani,sehemu za VIP za kuangalia mpira lakini na sehemu za Bustani kwaajili ya wageni waalikwa kufika na kupumzika katika mazingira mazuri.   Lakini pia kwa chini Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kupaki magari,kutakuwa na sehemu ya kumbi za sinema,kutakuwa na sehemu ya utalii na makumbusho ya timu hiyo ya Real Betis. Huko Hispania ni mwendo wa Viwanja vizuri tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live