Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eriksson atoa kauli ya mwisho akikaribia kifo

Sven Ericssson Eriksson atoa kauli ya mwisho akikaribia kifo

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa zamani wa England, Sven-Goran Eriksson ameaga familia ya mpira wa miguu kwa mara ya mwisho na kusema namna gani anataka watu wamkumbuke.

Eriksson anasumbuliwa na kansa ambayo haiwezi kupatiwa matibabu ya aina yoyote kwa vile imeshasambaa katika sehemu nzima ya mwili wake.

Kocha huyo amesema kuwa anafurahia maisha aliyoishi ya kutumikia mpira wa miguu.

“Nilikuwa na maisha mazuri. Nadhani wote tunahofia siku ambayo tutakufa. Lakini maisha ni kifo kiuhalisia.

“Unatakiwa kujifunza kukubaliana nacho kama kilivyo. Ninaamini mwishoni watu watasema yeah, alikuwa ni mtu mzuri, lakini sio kila mmoja atasema hivyo,” alisema Eriksson.

Kocha huyo raia wa Sweden alisema anaamini atakumbukwa kwa mazuri mengi.

“Nina tumaini mtanikumbuka kama mtu chanya niliyejaribu kufanya kila kitu anachoweza. Msiwe mnasema pole, tabasamuni. Asanteni wote kwa kila kitu, makocha, wachezaji na umati (mashabiki) ilikuwa ya aina yake. Jitunzeni nyie binafsi na tunzeni maisha yenu na muishi,” alisema Eriksson.

Chanzo: Mwanaspoti