Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eriksen: England ni bahati tu

Christian Eriksen Eriksen: England ni bahati tu

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Manchester United na Denmark, Christian Eriksen amesema England ilikuwa na bahati kutoka sare katika mchezo wa hatua ya makundi ya Euro dhidi yao uliopigwa Alhamisi ya wiki hii.

England ilionyesha kiwango kibovu katika mchezo huo wa kundi C hali iliyozidisha presha kwa kocha wao, Gareth Southgate anayetajwa huenda akafutwa kazi baada ya kumalizika kwa michuano hii inayopigwa huko Ujerumani.

Eriksen ambaye katika mechi hiyo alikuwa akicheza kama kiungo wa kati wa Denmark alisema England walifanya makosa zaidi ya alivyotarajia.

“Tulikuwa na nafasi za kufunga. Nafikiri tulipaswa kufunga na kushinda mchezo, hivyo kutoka sare ni jambo lililotusikitisha kidogo, tulikuwa bora kwa asilimia kubwa, tulicheza kutokea nyuma na kutengeneza nafasi, tuliwapa wakati mgumu katika mashambulizi ya kushtukiza na muda mwingi tulimiliki mpira,” alisema Eriksen.

“Tulikuwa na vipindi vizuri sana katika mechi, kijumla tulicheza vizuri na kuonyesha ubora tulionao, lakini hiyo haitufanyi tuone kama ndio tumemaliza, bado safari ni ndefu hadi pale tutakapocheza mechi ya mwisho.”

Kipa wa Denmark, Kasper Schmeichel naye alitamba walikuwa bora zaidi kuliko England na kubwa zaidi walikuwa na nidhamu sana uwanjani.

“Tulikuwa na nidhamu sana na tulionyesha hali ya kupambana muda wote, hatukuwa na woga licha ya kufahamu wana mtu kama Harry Kane ambaye ni kama sumaku, kosa dogo tu anakuadhibu.”

England na Denmark zote zimesonga mbele hatua ya 16 bora na England itaumana na Slovakia na Denmark itacheza na Ujerumani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live