Kocha wa klabu ya Manchester United Erik ten Hag amesema kuwa mchezo wa juzi dhidi ya Brighton wamepoteza kwa sababu ya kukosa kujiamini.
Erik ten Hag mchezo wake wa jumapili ndio mchezo wa kwanza kwenye msimu huu, na mchezo wake ufunguzi kwenye ligi kuu ya Uingereza, ambapo kikosi chake kimepokea kipigo cha goli 1-2, kwenye uwanja wake nyumbani na kuwa na mwanzo mbaya wa msimu.
Pascal Gross alifunga goli zote mbili kipindi cha kwanza, na baadae Manchester United walipata goli moja la kufutia machozi, ambalo nalo Alexis MacAllister alijifunga kwenye dakika 68, kufanya mchezo umalizike kwa 1-2.
Erik ten Hag akiwa anaongea na waandishi wa habari baada ya mchezo kuisha alinukuliwa akisema:
“Nadhani ulikuwa mwanzao mzuri na kisha baadae uwezo wa kujiamini ukashuka chini na tukafanya makosa na wapinzani wetu wakatuadhibu.
“Naweza kuelewa hilo kutojiamini baada matokeo ya mwaka uliopita lakini si muhimu. wachezaji wazuri lakini kujiamini kunaanza na wewe mwenyewe. Najua ingetokea lakini nadhani tungefanya vizuri, hilo liko wazi lakini haiwezekani kwa usiku mmoja.
“Leo tulikuwa na wakati mgumu kwenye kipindi cha kwanza na tunapaswa kujifunza kutoka kwenye hilo, na hilo liko wazi.”