Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Erik Ten Hag ampa neno zito Mason Mount

MM Contract EtH 31688570847534 Large Mason Mount na Erik Ten Hag

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Erik ten Hag amemwambia Mason Mount, 24, anamtaka awe mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Manchester United.

Kiungo mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England alisaini mkataba wa miaka mitano kwenye kikosi hicho cha Man United akitokea Chelsea wiki iliyopita.

Na sasa imethibitishwa, Ten Hag amemweka Mount kwenye orodha ya wachezaji muhimu kwenye kikosi chake, alipomwambia:

“Nataka uwe mchezaji muhimu kwenye timu.” Katika majibu, Mount alionekana kuwa tayari wakati aliposema: “Sawa bosi, asante. Nipo tayari.”

Mount atakwenda kuongeza mabao na asisti kwenye kiungo ya Man United, baada ya kufunga mara 58 na kuasisti 53 katika mechi 279 alizochezea klabu yake iliyopita.

Kuna matumaini makubwa Mount atakwenda kufanikiwa Man United ambako amekabidhiwa jezi Namba 7.Jezi hiyo iliwahi kuvaliwa na magwiji kama David Beckham, Bryan Robson, Eric Cantona, Cristiano Ronaldo na George Best.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live