Mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wameripotiwa kuwa na mpango wa kumletea Harry Kane mchezaji mwenzake wa zamani waliyekuwa pamoja Tottenham Hotspur, Eric Dier wakakipige huko Allianz Arena.
Miamba hiyo ya Bundesliga imeachana na mpango wa kumchukua staa wa Chelsea, Trevoh Chalobah na hivyo wamehamia kwa Dier wakiamini ndiye aliye kwenye mpango wa kocha Tuchel kwenye kuboresha safu yake ya mabeki.
Dier mwenye umri wa miaka 29, amejikuta hana nafasi kwenye kikosi cha Spurs tangu kocha Ange Postecoglou alipotua kwenye kikosi hicho.
Dier alihusishwa na mpango wa kuondoka dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini aliamua kubaki akiamini kwamba atapambania nafasi kwenye kikosi hicho.
Alicheza mechi 31 za ligi msimu uliopita, lakini msimu huu bado hajacheza dalkika yoyote.
Amejikuta hana nafasi kwenye kikosi Dier alihusishcha Spurs tangu kocha Ange Postecoglou alipotua kwenye kikosi hicho.
Staa mpya aliyesajiliwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi Micky van de Ven ndiye aliyempora namba Dier na ametengeneza kombinesheni matata kabisa na Cristian Romero kwenye safu ya ulinzi ya miamba hiyo ya London.
Kwa mujibu wa gazeti la Bild la Ujerumani, Tuchel anahitaji beki wa kati kwenye dirisha la Januari na ilikuwa ikitajwa Chalobah ni chaguo la kwanza kwenye mpango wake, kabla ya mambo kubadilika na sasa Dier amewekwa kwenye rada za wanaosakwa Allianz Arena.