Kiungo wa Chelsea anayefanya vizuri kwa sasa Enzo Fernandez huenda akawa moja kati ya wachezaji wenye umri mdogo zaidi kuchukua tuzo kubwa ya dunia.
Alifanya hivyo kwenye mashindano ya kombe la dunia 2022 nchini Qatar, kwa kutambuliwa kama mchezaji bora chipukizi baada ya timu yake ya taifa ya Argentina kutwaa taji hilo la dunia. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni.
Enzo Fernandez (22) mzaliwa wa maeneo ya San Martin, Buenos Aires ya huko Argentina na maisha yake ya soka yalianzia pale Club La Recova na baadae alijiunga na River Plate mwaka 2019 lakini alikuwa kwenye akademi ya timu hiyo mapema sana mwaka 2005.
Mwaka 2020-21 alitolewa kwa mkopo kwenda timu ya Defensa y Justicia hakukaa sana huko msimu wa 2022-23 alijiuga na klabu kubwa ya Benfica ambayo wengi walimfahamu huko kabla ya kujiunga na klabu ya Ligi kuu ya Uingereza ya Chelsea kwa dau kubwa la paundi milioni 106.8
Je Anaweza Kushinda Ballon d’or?
Kuna sababu kuu tatu zinaweza kumpatia ushindi wa tuzo kubwa kabisa dunia kwa wanasoka ya Ballon D’or nazo ni kama:
1.Ubingwa wa Kombe la Dunia 2022
Baada ya kutwaa ubingwa huo nchini Qatar Enzo Fernandez amejiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutwaa tuzo hiyo, inayowaniwa na wachezaji wengi zaidi ambapo kwa sasa Lionel Messi ndiye anayeoongoza kuchuka akiwa ametwaa mara 7 anafuatiwa na Cristiano Ronaldo nyota wa Ureno mwenye Ballon D’or 5.
2.Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukuzi wa WC 2022
Hii nayo huenda ikawa ni moja ya sababu nyingine kinda huyu mwenye miaka 22 akatwaa tuzo hiyo na kuandika rekodi nyingine ya dunia.
3.Ubingwa wa UCL na Chelsea
Baada ya Lionel Messi na Kylian Mbappe kuondoshwa kwenye hatua ya 16 bora, sasa ni kama nuru ya Enzo inang’aa kwa sababu bado Chelsea wapo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuiondosha Borussia Dortmund, na endapo Chelsea watachukua ubingwa huo wa UCL itaongeza sifa kwa nzo kuwana Tuzo ya Ballon D’or lakini lolote linawezakana Mbio za Messi na Mbappe bado zinaweza kuwa kikwazo kwa nyota huyo wa Chelsea.