Kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique inaelezwa anavutiwa na kufundisha katika ligi kuu ya Uingereza lakini inaelezwa amekigomea kibarua cha kufundisha klabu ya Tottenham Hotspurs.
Klabu ya Tottenham Hotspurs inaelezwa ilikua inahitaji huduma ya kocha Luis Enrique baada ya kuachana na kocha wake raia wa kimataifa wa Italia Antonio Conte, Lakini kocha wa huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona amekigomea kibarua cha klabu hiyo.
Kocha huyo wa kimataifa wa Hispania amekua kwenye rada za timu mbalimbali za ligi kuu ya Uingereza kwa kipindi kirefu ikiwemo Manchester United ambayo tayari imeshapata kocha kwasasa ambaye anafanya vizuri, Lakini kocha huyo kwasasa licha ya kuvutiwa na ligi kuu ya Uingereza atalazimika kusubiri kibarua kwenye timu kubwa baada ya kuikataa kazi ya Spurs.
Luis Enrique amekua kocha wa viwango kwa muda mrefu sasa akihudumia klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania kwa mafanikio makubwa, Hivo kufanya kua moja ya makocha wa heshima kubwa barani ulaya na wenye kuwindwa zaidi kutokana na ubora wake.
Baada ya kocha Luis Enrique kukataa kibarua cha kuitumikia klabu ya Tottenham Hotspurs ambaye imemuondoa kocha Antonio Conte aliyekua akifundisha timu hiyo, Kocha Lucho sasa atahitajika kuangalia timu nyingine ndani ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kukigomea kibarua cha klabu ya Tottenham kama taarifa zinavyoeleza.