Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

England yazima ndoto za Senegal, Afrika Kombe la Dunia

F8E2336D 06E1 496A B7E1 2CA7690165FF.jpeg Kiungo wa England, Henderson akiwaacha Senegal hoi baada ya kufunga bao la kwanza

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya England "Three Lions" imezima ndoto za Timu ya Taifa ya Senegal jana Disemba 4 baada ya kuichapa mabao 3-0 hatua ya 16 bora Michuano ya Kombe la Dunia.

Senegal ndio timu kutoka bara la Afrika ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kufanya vyema katika michuano hiyo na pengine kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufika nusu fainali ya michuano hiyo kutoka bara la Afrika.

Magoli ya England katika mchezo huo yamefunga na kiungo Jordan Henderson 38', Harry Kane 45+3 na Bukayo Saka kipindi cha pili dakika ya 57.

Kiungo Jude Belligham alionesha kiwango bora katika mchezo huo akitoa pasi ya bao kwa henderson lakini akihusika katika utengenezaji wa bao la pili la Harry Kane

Kuondolewa kwa Senegal kunafanya bara Afrika kubaki na mwakilishi mmoja tu ambae ni Morocco anaekabiliana na Hispania siku ya Jumanne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live