Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

England yafuzu kwenda Qatar 2022 kibabe

England Lions England yashinda magoli 10

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya England imejikatia tiketi ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022, baada ya ushindi wa 10-0 dhidi ya wenyeji, San Marino usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Olimpico Jijiji Serravalle.

Mabao ya Three Lions yalifungwa na Harry Maguire dakika ya sita, Filippo Fabbri aliyejifunga dakika ya 15, Nahodha, Harry Kane manne dakika za 27 kwa penalti, 31, 39 kwa penalti na 42.

Mengine yalifungwa na Emile Smith Rowe dakika ya 58, Tyrone Mings dakika ya 69, Tammy Abraham dakika ya 78 na Bukayo Saka dakika ya 79.

San Marino katika mchezo huo walijikuta wakicheza pungufu kwa zaidi ya dakika 30 baada ya beki wao Dante Carlos Rossi kuonyeshwa kadi nyekundu.

Hii ni mara ya kwanza England Iliyo chini ya kocha Gareth Southgate inafunga mabao zaidi ya tisa kwenye mechi moja tangu mwaka 1964 na inamaliza na pointi 26 na kufuzu fainali za Qatar kama kinara wa Kundi I ikiizidi pointi sita Poland ambayo sasa itakwenda kujaribu bahati katika Playoffs.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live