Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

England waanza kwa ushindi mnono Kombe la Dunia

England 6 England imeibuka na ushindi wa magoli 6-2

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabao 8 yamepatikana kwenye mchezo wa Kombe la Dunia huko Qatar baada ya dakika 90 kukamilika kati ya England dhidi ya Iran.

Ubao wa Uwanja wa taifa wa Khalifa umesoma England 6-2 Iran kwenye mchezo wa kundi B.

Mabao ya Jude Bellingham dakika ya 35, Bukayo Saka dakika ya 43 na 62, Raheem Sterling dakika ya 45+1, Marcus Rashford dakika ya 71 na msumari wa mwisho ulipigwa na Jack Grealish dakika ya 89.

Msumari wa Grealish ulikamilisha idadi ya mabao 6 huku yale mawili kwa Iran yakifungwa na Mehdi Tarem dakika ya 65 na 90+13 kwa mkwaju wa penalti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live