Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

England uso kwa uso tena na Italy

England Vs Italy Euro.jpeg England vs Italy

Sun, 9 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya England itakutana na timu ya taifa ya Italia kwa mara nyingine tena baada ya droo kuchezeshwa leo kuelekea michuano ya mataifa ya ulaya mwaka 2024.

Timu hizi zitakua zinakutana kwa mara ya nne katika vipindi vya hivi karibuni baada ya kukutana katika fainali ya michuano ya mataifa ya ulaya (Euro) mwaka 2021 na Uingereza kupoteza fainali hiyo kwa mikwaju ya penati, Pia walikutana mara mbili katika michuano ya Uefa Nations League ambapo walikua kundi moja.

England wamepangwa kundi moja na nchi za Malta,Ukraine,North Macedonia pamoja na Italia katika kundi C ili kuweza kufuzu michuano ya mataifa ya Ulaya mwaka 2024 yatakayofanyika nchini Ujerumani.

Michuano hiyo ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne yamewafanya Ujerumani kutokutokea kwenye makundi hayo yaliyopangwa baada ya kupata faida ya kua mwenyeji wa michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live