Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

England mikononi kwa Wajerumani UEFA Nations

0 Euro 2020 Round Of 16 England V Germany Mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger akijaribu kumzuia Bukayo Saka wa England

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: eatv.tv

Michuano ya Uefa Nations League inaendelea tena leo kwa michezo 6 kuchezwa huku michezo miwili ya kundi A 3 ikitarajiwa kuteka hisia za mashabiki wengi wa soka kwa Ujerumani kucheza na England kwenye dimba la Allianz Arena huku Italia wakicheza na Hungary usiku wa leo

Michezo mingine leo Finland watacheza na Montenegro,Bosnia & Herzegovina wakipambana na Romania,Faroe Islands dhidi ya Luxembourg huku Lithuania wakipambana na Uturuki huku michezo yote ikitarajiwa kuchezwa majira ya 21:45 usiku

Matokeo ya hapo jana mabingwa watetezi Ufaransa walibanwa na Croatia kwa kwenda sare ya bao 1-1 huku kiungo Andrio Rabiot akiwatanguliza les blues dakika ya 52 kabla Andrey Kramaric kusawazisha dakika ya 82 kwa mkwaju wa penati.

Chanzo: eatv.tv