Baada ya vurugu zilizofanywa na Mashabiki wake wasiokua na tiketi siku ya Fainali ya michuano ya Euro 2020, England inajiandaa kukabiliana na adhabu itakayotolewa na Chama cha Soka Ulaya (UEFA).
Kamati ya nidhamu ya UEFA, itaamua adhabu pale itakapokutana Jumatatu ya leo au Jumanne jioni.
Engaland wanatazamiwa kuadhibiwa kwa kucheza mechi moja ya nyumbani bila ya kuhudhuriwa na mashabiki kama sehemu ya adhabu kwa kile ambacho mashabiki wake walikifanya wakati wa Fainali ya Mataifa ya Ulaya(Euro).
Mashabiki wa Uingereza wasiokuwa na tiketi walisababisha vurugu kubwa pale walipoingia katika mvutano na walizi wa uwanja na polisi kwa kile walichokuwa wakilazimisha kwenda kutazama mchezo wa Fainali kati ya England na Italia.
Fainali ambayo iliisha kwa Italia kubeba ubingwa huo, baada ya kuibuka na ushindi kwa changamoto ya mikwaju ya penati.