Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi atoboa siri ya Yanga kufanya vizuri

Hersi Mwana Fa730 Eng. Hersi.

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said ametoboa siri ya timu yake kufanya vizuri kwa miaka ya hivi karibuni akisema kuwa wachezaji wanaowataka kwenye timu hiyo wanahakikisha wanawapata kwa thamani halisi wakati wa usajili wao.

Yanga kwa misimu miwili sasa imefanikiwa kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu na kucheza fainali ya CAFCC na robo fainali ya CAFCL huku wakibeba pia ubingwa wa Kombe la Shirikisho Tanzania kwa misimu miwili.

"Katika hali ya kawaida ukitaka kufanya vizuri lazima uwe na wachezaji wako bora na sisi kama Young Africans SC utaratibu wetu kwanza ni kuhakikisha tunamshawishi mchezaji anayetaka kuondoka abaki.

"Hatua ya pili kama mchezaji ameamua kuondoka lazima tuhakikishe tunamuuza katika bei sahihi ili Klabu inufaike na kuondoka kwake na hatua ya tatu ni kuziba nafasi yake kwa kununua mchezaji mwenye kiwango chenye ubora," amesema Hersi Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live