Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi atoa tafsiri ya nyota 3 kwenye jezi ya Ubingwa

Yangasc Bingwa 30 Eng. Hersi atoa tafsiri ya nyota 3 kwenye jezi ya Ubingwa

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Yanga Eng. Hersi Said ametoa tafsiri ya nyota 3 zinazoonekana kwenye T-shirt za ubingwa walizovaa wachezaji, viongozi na baadhi ya mashabiki wa Yanga SC baada ya kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara 2023-24.

Hersi amesema kwenye hizo nyota 3 ni tafsiri sahihi ya makombe 30 ya Ligi Kuu, kila nyota inabeba makombe 10.

Yanga wametwaa ubingwa wa Ligi msimu huu baada ya kuibuka na ushindi wa Mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugara jana jioni na kufikisha alama 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live