Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi amshukuru GSM baada ya ushindi

Herwi GSM 098793145 Eng. Hersi amshukuru GSM baada ya ushindi

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu katika mchezo wake dhidi ya Medeama katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Katika mchezo huo ambao Yanga imepata ushindi wa wa mabao 3-0, mchezo ulikuwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga ili kufufua matumaini ya kufuzu Robo Fainali.

Sasa baada ya ushindi huo kupitia ukurasa wa instagram wa Rais wa Young Africans, Hersi Said ameandika maneno haya kufuatia ushindi huo.

‘Imekuwa siku yenye baraka kwa #wananchi kwa zawadi ya ushindi mnono katika hatua ya makundi ya CAF CHAMPIONS LEAGUE.Ushindi huu unakuwa wa kihistoria huku soka safi likitandazwa mbele ya mashabiki bora’

‘Ama hakika, Ushindi huu ni zawadi kwa wana Yanga SC wote huku tukisherehekea GSM DAY, ambayo IMEFANA SANA nje na ndani ya uwanja.Kwa niaba ya wananchi nichukue fursa hii kukushukuru sana Mr. GHALIB kwa mchango wako mkubwa klabuni kwetu na wakati huu ukiwa huko katika ibada maalum ya UMMRA na familia yako, naamini umetuombea na kuiombea timu ya wananchi Yanga SC’-

.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live