Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi amalizana na Sankara Karamoko, sasa kutua Yanga

Karamoko Sankara Eng. Hersi amalizana na Sankara Karamoko, sasa kutua Yanga

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Yanga zinaeleza kuwa, uongozi wa timu hiyo umefikia makubaliano ya awali na mshambuliaji wa kati wa ASEC Mimosas, Sankara Karamoko.

Yanga wapo sokoni kwa sasa kusaka mshambuliaji atakayeweza kuvaa viatu vya aliyekuwa mshambuliaji wao, Fiston Kalala Mayele aliyetimkia Pyramids mwishoni mwa msimu uliopita na kumsajili Hafiz Konkoni ambaye bado hajaonyesha ubora ndani ya kikosi cha Gamondi.

Taarifa kutoka chanzo makini ndani ya Yanga kimesema kuwa, mshambuliaji huyo kama kila kitu kitakwenda sawa basi atajiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa katikati ya Desemba.

Sankara pia anavutiwa kujiunga na Yanga kutokana na uwepo wa Peodoh PacĂ´me Zouzoua, Stephanie Aziz Ki na Kouassi Attohoula Yao ambao walicheza wote ndani ya ASEC Mimosas.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live