Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi afungukia kumvuta straika Aziz Ki

Ki Aziz.jpeg Aziz Ki

Sat, 26 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya kuibuka kwa tetesi kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mpango wa kumsajili nyota wa Asec Mimosas ya Ivory Coast, Stephane Aziz Ki, Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Eng. Hersi Said ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambao ni wadhamini wa klabu hiyo, amefunguka ukweli wa jambo hilo.

Hersi aliweka wazi na kukubali kuwa ni kweli wamemuona nyota huyo na kukubali uwezo wake, ila ni ngumu kusema kuwa watamsajili kwa sasa kwa kuwa hawataki kukurupuka kwenye sekta hiyo na nguvu kubwa kwa sasa wamewekeza kwenye kulisaka taji la ligi kuu.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari juzi, Injinia Hersi alisema: “Ni kweli tuna idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwisho wa msimu. Hatukurupuki kuongeza mikataba, malengo yetu kwa sasa ni kombe la ligi kuu ili tupate nafasi ya kuiwakilisha nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live