Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi afunguka kuwa Mwenyekiti wa Simba

Hersiiiii Eng. Hersi afunguka kuwa Mwenyekiti wa Simba

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga Sc, Eng. Hersi Said amesema kuwa hawezi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba hata kama timu hiyo itamtaka akaihudumie.

Eng. Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na Clouds Media jana Jumatatu, Januari 8, 2024 kuhusu mambo mbalimbali ya Yanga na utendaji wake ndani ya klabu hiyo.

“Kwenye Levo ya klabu mimi ni mwanachama wa Yanga Sc na kwenye nafasi yangu nimechaguliwa na wanachama hivyo siwezi kuwa mwanachama wa klabu nyingine kwa sababu mimi ni Rais wa Yanga.

"Kama itahitajika limetokea dili nje ya klabu ya Yanga SC inamaanisha mimi nikawe mwenyekiti wa klabu husika, nafasi ambayo inahitaji idhini Kutoka kwa wanachama husika wa klabu hiyo.

"Kwa mfano mimi siwezi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba Sc kwa sababu mimi tayari ni mwanachama wa Klabu ya Yanga Sc, hivyo wanachama wa Simba Sc hawawezi kunipitisha mimi kwa kuwa sio mwenzao.

"Kwa hiyo kwa sasa kama ikitokea kuna klabu inanihitaji kunitoa Yanga ili nikawe mtendaji wao hicho kitu hakiwezekani,” amesema Eng. Hersi Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live