Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi afunguka alivyomnyofoa Chama ndani ya Simba

Hersi Chama Vdsxv Eng. Hersi afunguka alivyomnyofoa Chama ndani ya Simba

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa alimshawishi aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama na kufanikiwa kunasa saini yake baada ya kumaliza mkataba.

Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na Wasafi Media kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo klabu hiyo.

“Chama ni hatari, ninajaribu kumwangalia jinsi anavyoingia kwenye timu, ana uzoefu mkubwa na anaweza kuongeza thamani kubwa kwenye timu yetu. Chama ni mchezaji mwenye mafanikio makubwa kwenye CAFCL akiwa na mabao 19.

“Nilishawahi kuulizwa miaka miwili iliyopita kuhusu nafasi ya Chama ndani ya Yanga nikasema ni mchezaji naefaa kuja kucheza Yanga kwa ubora wa timu ambayo tumetengeneza hapaswi kucheza timu nyingine.

“Wakati msimu wa 2023/24 unamalizika nilimwambia ‘Chama ni Yanga pekee ndiyo timu unayoweza kucheza hapa nchini, njoo uje ucheze na watu ambao watayafanya maisha yako yawe rahisi. Huwezi kucheza timu ambayo umebeba mgongoni watu 10’.”

“Chama kwa nini alichagua kuja Yanga? Ni kwa sababu ni timu bora Afrika kwa sasa kuanzia wachezaji, benchi la ufundi na vifaa vya mazoezi. Chama akasema mimi ninataka kuja Yanga nimalizie carrier yangu kwenye kiwango bora, nikamwambia njoo. Sio timu ambayo usipopata matokeo unatukanwa, Yanga usipopata matokeo tunakwambia pumzika hapa wanaingia wengine na matokeo yanapatikana.

“Chama ilikuwa rahisi kwake kufanya maamuzi, na baada ya kusaini Yanga kabla hatujamtambulisha, zikaja ofa mara tatu ya ile ambayo alikuwa amesaini Yanga kutoka hapa Tanzania. Akanitumia ile ofa nikaiangalia nikaona ngoma ngumu lakini nikamweleza wewe ni professional umeshasaini, pili hizi pesa zinakuja wakati hawa watu hawakukutazama kipindi walichotakiwa wakutazame.

“Kulikuwa na majaribio mengi ya kutaka kumrejesha Chama arudi alikokuwa, lakini jamaa ni too professional, akasimamia msimamo wake, akasema ninafunga kila kitu na ninakuja Yanga kutumikia mkataba wangu,” amesema Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: