Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Yanga italeta ubingwa wa Afrika

Yanga Group Stage.png Eng. Hersi: Yanga italeta ubingwa wa Afrika

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa timu hiyo inaweza kuleta Ubingwa wa Afrika ndani ya miaka mitano endapo itaendelea na kasi hii ya kujiboresha na kufanya vizuri kwenye kila michuano inayoshiriki.

Kauli hii ya Eng. Hersi inakuja mara baada ya Yanga ambao ni washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25 huku wenzao Simba wakiwa wameshgiriki hatua hiyo kwa miaka mitano mfuflulizo.

“Nimejaribu kufanya tahmini zangu mwaka jana ilikuwa kidogo tu tulete Kombe la Afrika na hatukuweza kufanikiwa. Mwaka huu nimeanza kuifuatilia Ligi ya Mabingwa na kuona Yanga ina ubora kuliko vilabu vingi ambavyo vimeingia kwenye makundi ya CAFCL.

“Siwezi kusema ubora wa mwaka huu unaweza kutufanya tulete kombe lakini ndani ya miaka michache ijayo. Tunataka kwenda mbali zaidi na kuleta Kombe la Afrika kwenye ardhi ya Tanzania ndani ya miaka mitano ijayo kama tutaendelea kuijenga timu yetu kwa ubora huu.

“Kwa hii kasi tunayoenda nayo, inaweza kuwa chanzo cha kuleta kombe la Mabingwa Afrika hapa Tanzania,” amesema Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live