Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Yanga bado tunamdai Pacome

Yanga Kombe Mkapa.jpeg Eng. Hersi: Yanga bado tunamdai Pacome

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Young Africans, Eng. Hersi Said amewaambia Wananchi kwamba bado kiungo wao, Pacome Zouzoua tuna mdai pakubwa sana.

Eng. Hersi amesema kutokana na uwezo mkubwa alionao Pacome raia wa Ivory Coast, msimu huu ameuonyesha kidogo hivyo bado ana deni kubwa la kulipa.

“Huyu bado tunamdai sana, kama kuna mchezaji mwenye uwezo na hajatuonyesha uwezo wake kwa inavyotakiwa ni huyu, hivyo bado tunamdai.

“Huyu Pacome tunamdai, huyu akicheza kwa kiwango chake kile cha juu hakuna atakayemsogelea Afrika sio Tanzania pekee,” alisema Eng. Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live