Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Yanga bado hatujamalizana na Simba, bao 6-0 lazima zilipwe

Hersi Said.png Eng. Hersi: Yanga bado hatujamalizana na Simba, bao 6-0 lazima zilipwe

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa timu hiyo bado haijamaliza kulipa deni la kipigo kikubwa kutoka kwa watani zao Simba SC, hivyo kabla ya kuondoka madarakani atakahikisha visasi vyote vinelipwa.

Simba na Yanga watashuka dimbani leo kuwania alama tatu katika ligi kuu ya NBC kunako dimba la Benjamin Mkapa huku Simba wakiwa na kumbukumbu ya kupokea kipigo kizito cha bao 5-1 mwezi Novemba mwaka 2013.

"Hatujamalizana na Simba bado wanatudai boli 6 za mwaka 1977. Zile goli 5 zilikua ni deni la 2012 bado hilo deni walilokopeshwa wazee wetu zamani tutawalipia in shaa Allah.

"Chini ya uongozi wangu nitahakikisha kila deni la Yanga linalipwa hata kama ni deni la karne iliyopita," amesema Hersi.

Itakumbukwa kuwa, mwaka 2012 Simba iliifunga Yanga bao 5-0, lakini miaka 35 kabla ya hapo, yaani mwaka 1977, Simba iliwahi kuifunga Yanga bao 6-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live