Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Tutatafuta mbadala wa Mayele

MAYELE TRE.jpeg Fiston Mayele

Sun, 16 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga umefikia makubaliano ya kumuuza nyota wao wa kimataifa wa DR Congo, Fiston Mayele baada ya nyota huyo kuonyesha nia ya kutaka kuondoka, huku mabingwa hao wakisaka mbadala wake wa kusaidiana na Kennedy Musonda.

Mayele ambaye alikuwa mfungaji bora Ligi Kuu akifunga mara 17, akiwa pia kinara wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) akifikisha mabao saba, anatakiwa na timu za AL Qadisiyah ya Saudi Arabia na Pyramids ya Misri.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili imezipata, zinadai kuwa uongozi wa Yanga umepokea ofa ya Dola 40,000 kutoka kwa moja ya timu hizo, ambayo ni suala la muda tu kumalizana na mchezaji huyo pamoja na uongozi wa timu.

Wakati Mayele akikaribia kuondoka Yanga, miamba hiyo ina majina manne mezani ya mshambuliaji ambaye anaweza kuvaa viatu vya mfungaji bora huyo mara mbili wa klabu, likiwamo la Makabi Lilepo wa Al Hilal ya Sudan, mwenye mkataba wa mwaka mmoja na timu yake.

"Mchezaji kaonyesha nia ya kuondoka na klabu ambazo zinamtaka zimefika mezani, baada ya kukaa na Mayele kwa zaidi ya mara tatu, ametuhakikishia kuwa anataka kuondoka, hivyo uongozi umeridhia hilo," alisema mmoja wa viongozi wa Yanga, jana.

Taarifa hizo zilisema, uongozi tayari umeweka ofa mezani juu ya Mayele, hivyo klabu inasubiri uamuzi wao kama watarudi watakuwa tayari kuondoka na nyota huyo aliyeipa Yanga mataji sita.

Klabu ya AL Qadisiyah, ambayo imetajwa kumhitaji Mayele, ndiyo ambayo Mtanzania Simon Msuva na nyota wa DRC, Walter Bwalya wanaitumikia.

Akizungumzia taarifa za kutaka kuondoka kwa nyota huyo, Rais wa Yanga, Hersi Said, alisema Mayele ni mchezaji bora na klabu hiyo ina furaha kuona akihusishwa kutakiwa na timu nyingine.

Hersi alisema hatua hiyo inaonyesha kuwa Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wakubwa ambao wanatazamwa na klabu kubwa, hivyo suala lake likiwa tayari taarifa zitatolewa, kwa sasa timu inaendelea na maandalizi ya msimu mpya.

“Kama atakuwa anataka kuondoka, tutaangalia vitu vitatu, moja tutataka kumbakiza, mbili tutaangalia bei nzuri, tatu ni nani atachukua nafasi yake," alisema Hersi katika moja ya mahojiano yake jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live