Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Tutaongeza wachezaji wapya dirisha dogo

Arafat Haji X Hersi Oktoba 25 Eng. Hersi.

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa wanatarajia kusajili wachezaji wapya kwenye dirisha dogo la usajili ili kuendelea kuimarisha kikosi chao msimu huu.

Hersi amesema hayo kufuatia mwendelezo mzuri wa matokeo ambao Yanga wanaupata kwenye Ligi Kuu ya NBC ambayo wapo kileleni na hasa baada ya kuwafunga watani zao Simba kwa bao 5-1 na jana kuwafunga Coastal Union kwa bao 1-0.

“Dirisha dogo wategemee ongezeko la Wachezaji kwa baadhi ya maeneo kwakuwa tayari tumeshakaa na Mwalimu pamoja na benchi lake kutambua maeneo hayo, kifupi kuendana na ratiba ngumu tutarajie usajili wa baadhi ya wachezaji wapya,” amesema Eng. Hersi.

Yanga sasa inatarajia kujiandaa na michezo ya Klabu bingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi ambapo imepangwa na Al Ahly, CR Belouizdad na Medeama.

Tangu kuondoka kwa mshambuliaji Mkongomani, Fiston Mayele aliyetimkia Pyrmaids FC, Yanga bado haijapata mshambuliaji sahihi wa kuziba pengo lake.

Licha ya kumsajili Hafizi Konkoni bado hajaonyesha kile ambacho wananchi walikitarajia kutoka kwake huku beki Gift Fred wa Uganda aliyeingia kikosini hapo msimu huu naye akikosa nafasi ya kuanza hivyo wawili hao ndiyo wanapewa nafasi kubwa ya kuachwa wakati wa dirisha dogo la usajili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: