Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Tunamhitaji Fei Toto

Fei Toto Hersi Mz Eng. Hersi: Tunamhitaji Fei Toto

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa kiungo wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' ni miongoni mwa wachezaji bora nchini Tanzania, hivyo yeye kama kiongozi wa soka na mdau wa soka anatamani kumuona mchezaji huyo akifanya vizuri kadri siku zinavyokwenda.

Hersi ambaye kipindi cha nyuma aliwahi kutajwa na Fei Toto kuwa ndiye sababu ya yeye kuondoka klabuni hapo, amesema kuwa hajawahi kuwa na shida na mchezaji huyo kutoka Visiwani Zanzibar.

“Feisal ni Bora ya wachezaji bora tulio nao kwenye Ligi yetu, mimi namjua binafsi ni kijana mzuri, kwenye maisha yangu sijawahi kuwa na shinda na Feisal na yeye analijua hilo.

“Sitaki kuhukumu yaliyopita mimi ni kiongozi wa mpira tunamuhitaji kwenye maendeleo ya Taifa letu tunamuhitaji kwenye vilabu vyetu, tunamuombea Mungu afanye vizuri ni hazina kwenye Timu yetu.

“Siku ya fainali ya Ngao ya Jamii tulipocheza na Azam FC, nilikutana na Fei Toto nikamueleza kuwa ni mchezaji mzuri na nikamtakia mema kwenye msimu mpya ujao,” amesema Eng. Hersi Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: