Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Tumewaacha mbali wapinzani wetu

Aziz KI X Ushindi Yanga Eng. Hersi: Tumewaacha mbali wapinzani wetu

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Young Africans SC, Eng. Hersi Said, amefichua kwamba, kwa namna uwekezaji uliofanyika klabuni hapo, ni wazi wamewaacha mbali sana wapinzani wao.

Eng. Hersi alibainisha kwamba, kutokana na kuwaacha mbali wapinzani, ndiyo maana wanapocheza dhidi yao katika michuano tofauti, wanakuja na mfumo wa kujilinda zaidi kutokana na kuiheshimu Young Africans.

“Kwa sasa hakuna Klabu Tanzania inayoweza kuisogelea Young Africans SC kwenye ubora, tumewaacha mbali. Ndio maana timu nyingi zikicheza na sisi zinakuja na mfumo wa kuzuia zaidi ikimaanisha wanaiheshimu Klabu yetu. Malengo yangu makubwa ni kuhakikisha Klabu yetu inakuwa moja ya Klabu bora Afrika,” alisema Eng. Hersi.

Msimu huu mpaka sasa, timu Young Africans ipo katika mbio za kutetea mataji yake mawili ya Ligi Kuu ya NBC na Kombe la FA ambapo ndani ya ligi kuu, wapo kileleni, wakati Kombe la FA wakiwa hatua ya robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: