Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Tulimpiga Simba hizoo... tano!

Hersiii WA0017 Eng. Hersi: Tulimpiga Simba hizoo... tano!

Sun, 12 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jioni ya jana imefanyika hafla fupi ya chakula cha jioni katika Jiji la Johannesburg, hafla hiyo maalum iliandaliwa na Rais wa CAF Patrice Motsepe akimkaribisha Rais wa FIFA Gianni Infantino nchini Afrika Kusini.

Viongozi wakubwa wa mpira Duniani wamehudhuria hafla hiyo akiwemo Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Ally Said ambapo amekutana na Rais Infantino akiwa na Mwenyeji wake Rais Motsepe.

Miongoni mwa mambo ambayo Rais wa FIFA Gianni Infantino aliyauliza Hersi ni matokeo ya ‘Derby’ ya Kariakoo iliyochezwa November 5, 2023 ambapo Hersi alimjibu kuwa waliipiga Simba bao tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live