Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Simba hawajatushawishi Kimataifa

Yanga Rekodi Mpyaaaaa.jpeg Eng. Hersi: Simba hawajatushawishi Kimataifa

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa wapinzani wao, Simba SC hawajawashawishi chochote kufanya vizuri kimataifa bali wao wamekuwa wakishawishia na ubora wao waliokuwa wameuweka tangu miaka ya nyuma.

Kauli hii ya Eng. Hersi inakuja mara baada ya Yanga kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25 huku wenzao Simba wakiwa wameshgiriki hatua hiyo kwa miaka mitano mfuflulizo.

“Niwapongeze Simba kwa kuingia makundi ya CAFCL, pia pole kwa Singida FG kwa kushindwa kufanya vizuri kimataifa. Yanga inakuwa inspired na Yanga yenyewe wala haiwezi kuwa inspired na mafanikio ya klabu nyingine yoyote hapa Tanzania.

“Hakuna mtu anaweza kutu-inspire hapa Tanzania kwa kuwa na mafanikio kuliko Yanga. Sisi tumekuwa na mafanikio makubwa ambayo ndiyo yamekuwa yaki-inspire timu nyingine kuwa kama sisi. Yanga ni mabingwa wa Tanzania kwa mara nyingi kuliko timu yoyote, kwa hiyo kama kuna mtu anapaswa kujifunza basi ajifunze kwa Yanga.

“Kwenye mashindano ya Kimataifa Yanga tumecheza fainali, na ni klabu ya kwanza kucheza robo fainali ya CAFCl kuliko klabu nyingine yoyote Tanzania.

“Tunachokifanya sasa hivi sio kuwa inspired na klabu nyingine badala yake ni kurejesha standard yetu na kwenda mbali zaidi, hii standard ilikuwepo kipindi cha nyuma.

“Yanga ili-set standard huko nyuma, kucheza robo fainali ya CAF, kwa hiyo kwetu sisikucheza robo fainali sio mafanikio ambayo tunajifunza kwa mtu mwingine, ni jambo ambalo lipo kwenye historia ya klabu yetu,” amesema Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live