Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Pesa ni tatizo kwa vilabu vingi

Eng Hersi Cafff Eng. Hersi: Pesa ni tatizo kwa vilabu vingi

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Young Africans, Eng. Hersi Ally Said amesema kuwa suala la kipato limekuwa tatizo kubwa kwa vilabu vingi vya soka Duniani, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya soka.

Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Al Ahly mjini Cairo, nchini Misri ambako timu yake imekwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Ukizungumzia uwezo wa kifedha ni tatizo kubwa la vilabu vingi duniani, kwa upande wetu tuna vyanzo kadhaa vya mapato kama Klabu. Moja ni udhamini, tuna wadhamini ambao wanatudhamini na kutupatia fedha, lakini chanzo cha pili ni Wanachama na Mashabiki.

"Tuna mfumo thabiti wa kuwawezesha makundi haya kuchangia Klabu ambapo husaidia kwenye gharama za uendeshaji na nichukue fursa hii kuwapongeza Wanachama na Mashabiki wetu kwa mchango wao.

"Hakuna namna unaweza kuwa timu bora bila kuwa na uwezo wa kifedha, hivyo pia niwashukuru wadhamini wetu Sportpesa ambae ni mdhamini mkuu, GSM Group Of Companies ambao ni wazalishaji na wasambazaji wa jezi zetu nchini, Whizmo, Hero, NIC Insurance pamoja na Azam Media ambao ni shirika kubwa la utangazaji Tanzania," Rais wa Young Africans Eng.Hersi Ally Said @alahlytv

Chanzo: www.tanzaniaweb.live