Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Ni mchezaji mmoja tu ambaye sijamsajili mimi Yanga

Inj Hersi Said M.jpeg Eng. Hersi Said.

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said wachezaji wote wa timu hiyo amewasajili kasoro kipa namba mbili, Metacha Boniphace Mnata lakini wengine wote wamepita mezani kwake.

Hersi amesema kuwa, wachezaji wote wa Yanga ni wachezaji wake ndiyo maana hawana matabaka ndani na nje ya uwanja na wote wanafanya kazi kwa kushirikiana ili kufikia malengo ya klabu.

"Katika kikosi cha Yanga ni mchezaji mmoja tu ambaye sijahusika kwenye usajili wake ambaye ni Metacha Mnata kwa sababu wakati naingia na Yanga nilimkuta. Wote wamepita mezani kwangu.

"Hivyo hakuna mchezaji ambaye kwangu ana thamani kuliko mwingine. Mchezaji yeyote anayecheza timu hii ya Yanga ni mchezaji wangu. Nina thamini wachezaji wote waliopo hapa bila kujali amesajiliwa na nani," amesema Eng. Hersi Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: