Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Mimi sio mwajiliwa wa Yanga, sipati hata shilingi 100

Eng. Hersi Sdv Eng. Hersi Said.

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa yeye sio mwajiliwa wa klabu hiyo wala hapati mshahara kutokana na kazi yake ndani ya klabu hiyo bali anachokifanya ni kuisimamia klabu.

Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na Wasafi FM kuhusu mambo mbalimbali kuhusu Klabu hiyo hususani mgongano wa kimaslahi baina ya Klabu hiyo na mdhamini wao GSM hasa ikikumbukwa kuwa Hersi alikuwa ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM kabla hajatua Yanga.

"Mimi sio mfanyakazi wa Yanga na sipati hata shilingi kutoka Yanga, hata kwenye mfumo wa mishahara ya wafanyakazi wa Yanga mimi sipo. Mimi na wajumbe wa Bodi ya wadhamini Mama yetu Fatuma Karume, Mzee Mkuchika, Mwigulu Nchemba, Tarimba Abbas hatupati hata shilingi mia kutoka Yanga, tunaisimamia Klabu.

"Mimi nina Biashara zangu binafsi ndio ambazo zinaniingizia kipato na sio Yanga, pale Yanga mimi ni Rais wa Klabu na sio mfanyakazi wa Klabu, mfanyakazi kazi wa Klabu anaanzia CEO hapo ndio level ya wafanyakazi ndani ya Klabu yetu inaanzia.

"Kama kuna jambo ambalo Wanayanga wanapaswa kuliombea dua liendelee ni uwepo wa GSM kwenye timu yetu, amekuwa akitusapoti katika mambo mengi mno.

"Mfano juzi kwenye Ngao ya Jamii kabla ya kuwashughulikia watu flani, alikuja na kutuuliza bajeti ya bonasi ikoje, tulipomwambia akasema haitoshi, akaongeza fungu la maana vijana wakaenda kupambana tukashinda," amesema Rais wa Young Africans SC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live