Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Malengo ya Yanga ni kucheza Kombe la Dunia la Vilabu

Yanga 699 1024x627.jpeg Eng. Hersi: Malengo ya Yanga ni kucheza Kombe la Dunia la Vilabu

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Young Africans SC, Eng. Hersi Said, amesema matamanio yake makubwa ni kuona msimu ujao timu inaingia kwenye orodha ya timu nne ili kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu.

Eng. Hersi amesema hayo kwa kubainisha kwamba, kama mwaka jana wamecheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na msimu huu wamecheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, basi wakiweka nia, yote yanawezekana.

“Matamanio yangu ni kuona mwakani kwenye mashindano ya Kimataifa tufike katika orodha ya timu nne bora AFRIKA, ili tuweze kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu. Mwaka jana tumefika fainali na tumepata alama nyingi ambazo zitatuongezea nguvu ya kushiriki Kombe hilo,” alisema Eng. Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live