Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Kuna watu walimshawishi Mzize avunje mkataba na Yanga

Clement Mzize Clementinho Eng. Hersi: Kuna watu walimshawishi Mzize avunje mkataba na Yanga

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa watu baadhi ya viongozi wa soka wanaoheshimika walitaka kumshawishi mshambuliaji wao Clement Mzize ili avunje mkataba na ajiunge nao.

Hersi amesema kuwa watu hao walijifanya kama wasimamizi wa Mzize na kupeleka barua Jangwani ya kuomba kuvunja mkataba jambo ambalo Mzize aliwakana na kuueleza uongozi wa klabu kuwa hawatambui.

“Mzize ni moja ya wachezaji waliotoka kwenye Under 20 ya klabu yetu, ni miongoni mwa vipaji bora ambavyo tuko navyo kwenye taifa letu na sisi kama Yanga ninaamini Mzize ni tegemeo la taifa letu na yuko kwenye mikono salama ya kumfanya mwaka 2027 tumtegemee kwenye AFCON.

“Vipo vilabu vingi ambavyo vimetaka kumchukua lakini sisi tunataka aendelee kuwa bora mpaka afike level ya kwenda kufanya makubwa nje na sio kwenda kujifunza. Bado ni kijana na ana vingi vya kujifunza na kufanya makubwa.

“Kuna mtu alileta ofa kubwa Afrika Kusini akisema hii ndiyo timu anatakiwa aende, lakini sisi tulipoenda pale tukawashona wale jamaa. Tukasema mbona tunaambiwa kama anaenda kucheza Man City lakini hii timu sisi Yanga tumeiacha mbali, tunacheza CAFCL, ni klabu kubwa na tuna nafasi ya kubeba ubingwa wa CAFCL. Kuna vilabu ndiyo vinajijenga lakini vinamtaka Mzize.

“Kuna ofa za hovyo kabisa ambazo tumewahi kuzipokea kuhusu Mzize na lengo lake ni baya sana. Kiongozi mkubwa kabisa na ana heshima zake kwenye soka, anamshawishi mchezaji avunje mkataba arudishe signing fee na mshahara wa miezi mitatu.

“Kwa bahati mbaya ile barua imekuja hata bila mchezaji mwenyewe kujua, wamejifanya kama ndio wasimamizi wa mchezaji wakaleta barua ya kuvunja mkataba. Uzuri mchezaji yule anajielewa, alisema viongozi wangu mimi huyu mtu simjui na achaneni nae, nitaendelea kuitumikia Yanga na kuutumikia mkataba wangu,” amesema Hersi.

Aidha, Hersi amesema kuwa watu hao walienda mbali zaidi na kumshawishi Mzize agomee mazoezi ya Yanga na hata kugomea kwenda pre-season nchini Afrika Kusini lakini kinda huyo alisimama kwenye msimamo wake na kukataa kushawishiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: