Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Fainali CAFCL itakuwa ya Al Ahly na Mamelodi

Al Ahly Vs Sundowns Eng. Hersi: Fainali CAFCL itakuwa ya Al Ahly na Mamelodi

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng Hersi Ally Said amesema kuwa, Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu itapigwa kati ya Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Hersi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu Barani Afrika amesema hayo nchini Misri wakati akiwa katika mahojiano na Televisheni ya Al Ahly kuhusu mambo mbalimbali ya Klabu ya Yanga na soka la Afrika kwa ujumla wake.

"Binafsi naamini fainali ya CAF Champions League msimu huu ni baina ya Al Ahly dhidi ya Mamelodi Sundowns. Al Ahly na Mamelodi ni timu zenye mikakati na ubora wa hali ya juu kwasasa Barani Afrika.

Hersi aliendelea kusisitiza, “Ikumbukwe Al Ahly ndio timu yenye uwekezaji mkubwa sana tena inapofika hatua za mtoano katika michuano hii, huku Mamelodi wakiwa ni mabingwa AFL na sidhani itakuwa rahisi kwao kuishia robo au nusu fainali," amesema Eng. Hersi Said.

Nini maoni yako kuhusu hili, utabiri wa Hersi upo sahihi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live