Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: Aliye nyuma ya mafanikio ya Yanga ni huyu!

Hersi Fa835 Eng. Hersi: Aliye nyuma ya mafanikio ya Yanga ni huyu!

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Young Africans, Eng. Hersi Ally Said amesema kuwa, mtu aliyeko nyuma ya mafanikio ya Klabu hiyo ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Al Ahly mjini Cairo, nchini Misri ambako timu yake imekwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Chachu ya mafanikio ya mpira wetu Tanzania ni Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye soka la nchi yetu.

Taifa Stars kufuzu kwenda kwenye fainali za AFCON 2023 nchini Ivory Coast ni moja katika mafanikio yake.

Kufaulu kwa UMOJA BID katika kuandaa AFCON 2027 ni sehemu kubwa ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha mchango wake mkubwa katika kujenga Hamasa kupitia “GOLI LA MAMA” umeifikisha Young Africans katika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika 2022/23 na sasa Young Africans kufuzu kwenda robo fainali ya Klabu bingwa barani Afrika.

Asante Sana Mama" Amesema Rais wa Young Africans Eng.Hersi Ally Said kwenye Kituo cha Televisheni cha @alahlytv Cairo, Egypt

Chanzo: www.tanzaniaweb.live