Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi Afunguka GSM Kulipa Mishara Yanga

Hersi Said.png?fit=640%2C420&ssl=1 Eng. Hersi Said

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya stori zilizopo mtaani kwamba Kampuni ya GSM ndiyo inalipa mishara wachezaji, viongozi na watumishi wa Klabu ya Yanga, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Mhandisi Hersi Said ameamua kuvunja ukimya na kufunguka ukweli.

"TIMU hizi zinajiendesha kwa hasara kwa miaka mingi ndio maana zimekwama. Ukisema hivi mtu anaweza asikuelewe lakini ukitazama mapato ya klabu na matumizi ndio utajua kwanini zinajiendesha kwa hasara.

"Yanga inalipa mishahara yenyewe, ina mifumo yake ya kuajiri watu sisi tuna-support tu. Yanga timu kubwa huwezi kufananisha na makolo. Huwezi kumleta mchezaji kama Bangala halafu hajui analipwa na nani.

"Tumechagua mfumo wa wanachama na wawekezaji. 51% kwa wanachama na 49% kwa wawekezaji. Hili tumejifunza La Liga na ndio maana unaweza ukaona kwanini Real Madrid na Barcelona zinapendwa na watu duniani. Tumejifunza kitu kikubwa sana," Eng. Hersi Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live