Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Enekia amfuata Ronaldo Saudia

Enekia Saudi Enekia amfuata Ronaldo Saudia

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Hatimaye staa wa Twiga Stars Enekia Kasonga amesafiri leo kuelekea nchini Saudi Arabia kujiunga na timu yake mpya Eastern Flames inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini humo.

Enekia ambaye awali ilikuwa ajiunge na Krybas ya Ukraine, ikashindikana kutokana na masuala ya Visa, ametua Flames kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Hii inakuwa timu yapili nje ya mipaka ya Tanzania kutumikiwa na staa huyu tangu aanze kucheza soka nje ya mipaka ya Tanzania.

Kwa mara ya kwanza Enekia alisajiliwa na Ausfaz inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Morocco mwaka 2021, ambako katika msimu wake wa kwanza alifanikiwa kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa ligi hiyo nakuwa mfungaji bora namba mbili kwa kufunga mabao 27.

Enekia anaungana na mastaa kibao ikiwemo staa wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo ambaye pia anacheza soka la kulipwa nchini humo kwenye klabu ya Al Nassr.

Chanzo: Mwanaspoti