Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Emoji za nyani zamponza Garnach0, Onana amtetea

Screenshot 20231026 185346.png Emoji za nyani zamponza Garnach0, Onana amtetea

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Soka England (FA) kinachunguza posti ya mchezaji wa Manchester United, Garnacho kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) akimpongeza kipa wao Andre Onana kwa kuokoa penalti kwenye mechi ya UEFA dhidi ya Copenhagen akitumia emoji za nyani (kama inavyoonekana pichani).

Baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo Onana ameomba jambo hilo lisifike mbali kwakuwa yeye hajachukizwa kwakuwa amemuelewa Garnacho akimaanisha ni nguvu na umoja.

Sakata kama hilo liliwahi kumkuta staa Edinson Cavani alipotumia neno 'negrito' kwenye Instagram ikitafsiriwa kuwa 'mtu mweusi' na kupelekea kufungiwa mechi tatu na kutozwa faini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live