Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Emilio Nsue: Nimefurahia kiwango AFCON 2023

Emilio Nsue Equatorial Emilio Nsue

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa timu ya taifa ya Guinea ya lkweta, Emilio Nsue ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga ‘hat-trick’ katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), tangu mwaka 2008.

Nsue mwenye umri wa miaka 34, alifunga hat-trick katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Guinea Bissau ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 4-2.

Nsue ndiye mchezaji anayeongoza kwa kupachika mabao matano katika michuano hiyo hadi sasa na ni mchezaji pekee aliyefunga ‘hat-trick’ msimu huu.

Staa huyo amekuwa mchezaji wa 17 kufunga ‘hat-trick tangu michuano hiyo ilipoanzishvwa mwaka 1957 ambapo fainali zilifanyikia nchini Sudan.

Straika huyo alishiriki fainali za mwaka 2015 na 2021 alifunga bao moja pekee katika misimu miwili.

Nsue alisema anafurahia kuonyesha kiwango bora na kuisaidia timu kufanya vizuri katika michuano hiyo msimu huu ambayo itakuwa ya mwisho kwake.

“Ninafurahia kiwango bora katika michuano msimu huu ambapo nimeisaidia timu yangu kuvuka hatua ya makundi.

“Michuano hii ya nitahakikisha kuonyesha itakuwa mwisho kwangu na ninafanya vizuri zaidi katika mechi zitakazofuata,” alisema Nsue.

Katika msimamo wa Kundi A, Guinea ya Ikweta imemaliza hatua ya makundi ikiwa kileleni kwa kujikusanyia pointi saba sawa na Nigeria wakati lvory Coast ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi tatu huku Guinea Bissau ikiburuza mkia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live