Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Emiliano Nsue: Viongozi wa Soka Guinea wametapeli fedha zetu

Emilio Nsue Equatorial Emilio Nsue

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa timu ya Taifa ya Equatorial Guinea Emilio Nsue baada ya kufungiwa na shirikisho la soka la nchi hiyo ametoa shutuma nzito kwa shirikisho la soka la nchi hiyo akidai wamekula pesa iliyokuwa kwa ajili ya timu ya Taifa.

"Shirikisho letu la Mpira (Equatorial Guinea) walizunguka kwa watu Mashuhuri na wenye Fedha wakawaambia waichangie Timu ya Taifa iliyopo AFCON lakini hatukuona kazi ya pesa hizo, hata jezi za Timu ya Taifa tukiwa kambini tulifua sisi wenyewe".

"Naumia kwa sababu ile sio Timu yetu pekee ni Timu ya wote lakini mzigo wote walituachia sisi na bado wameona haitoshi wakaamua kunifungia kisa nasema ukweli".

"Pesa zote mlizochanga kwa ajili yetu tukiwa Ivory Coast mmetapeliwa.Hatujaona faida yake na zimeliwa na maofisa mliowaamini ndani ya Shirikisho."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live